• Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Masasi District Council
Masasi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Asili ya Masasi
      • Historia ya Masasi Kiutawala
      • Orodha ya Viongozi
      • Ukubwa wa eneo
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi wa Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Ugavi na Ununuzi
      • Sheria na Usalama
      • Nyuki
      • Tehama na Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Agriculture
    • Construction Minerals
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Upimaji wa Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Utawala na Mipango
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
      • Elimu Afya na Maji
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • Jarida
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA MAONESHO YA NANENANE 2018 KANDA YA KUSINI

Posted on: August 8th, 2018

Halmashauri ya Wilaya Masasi Mkoani Mtwara imeibuka mshindi wa kwanza wa maonesho ya Nanenane kanda ya kusini kwa mwaka 2018  kati ya Halmashauri 15 za Mikoa ya lindi na Mtwara zilizoshiriki maonesho hayo yalifanyika  katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi baada ya kuwa banda bora kwa kuonesha tekinolojia kwa vitendo za Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Wajasiliamali na watumishi  wakishangili ushindi katika Maonesho ya Nanenane  kanda ya Kusini yaliyofanyika katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi tarehe 08.08.2018

Ushindi huo umetokana na banda hilo kuweza kutafsiri kwa vitendo kauli  mbiu ya maonesho hayo ya “kuwekeza katika Kilimo mifugo na uvuvi kwa maendeleo ya viwanda” ambapo teknologia za kisasa zilioneshwa katika mashamba darasa ikiwemo faida za matumizi sahihi ya Pembejeo kama mbegu za kisasa na viwatilifu ili kuwa na uzalishaji wenye tija utakaopekelea viwanda kuwa na malighafi za kutosha.

Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Masasi pia iliweza kuonesha kilimo jumuishi ambapo watu wenye ulemavu nao wanaweza kushiriki katika kujenga uchumi wa nchi kupitia shughui za kilimo cha busitani wakiwa nyumbani kwa kutumia vifaa rahisi kama makopo, mifuko mataili na vitu vingine ambapo wanaweza kuhudumia kwa urahisi bila kwenda mashamba ya mbali.

Kilimo cha Bustani ya Mbogamboga inayojumuisha makundi ya watu wenye mahitaji  maalumu (walemavu)

Mbali na kuwa mshindi wa kwanza kwanza kati ya Halmashauri 15 za Mikoa ya Lindi na Mtwara katika maonesho hayo, Halmasauri ya Wilaya ya Masasi imekuwa   mshindi wa pili wa jumla katika kilele cha maonesho hayo huku Jeshi la Kujenga Taifa likiibuka mshindi wa kwanza wa jumla.

Kutokana na ushindi huo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mhe. Juma Satmah, amepongeza Idara ya kilimo, watumishi na wajasilimali wote walioshiriki katika maonesho hayo kwa mchango wao uliofanikisha ushindi huo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mhe. Juma Satmah akipokea kikombe cha ushindi (aliyevaa koti) kutoka kwa mgeni rasmi wa sherehe hizo  Mhe Naibu Waziri wa TAMISEMI Joseph Kakunda (mwenye tisheti la kijani)  katika kilele cha maonesho ya Nanenane  kanda ya kusini yaliyofanyika katika viwanja vya Ngongo manispaa ya Lind. kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara mhe Gelasius Byakanwa

“Nawapongeza sana wote mlioshiriki katika maonesho haya hasa idara ya kilimo waliosimamia upandaji wa mazao kwenye mashamba haya ambayo yamefanya Halmashauri kuweza kuelezea uwekezaji wa  kilimo, mifugo na uvuvi kisasa kwa vitendo kwa ajili ya kuzalisha malighafi za Viwanda na hatimaye kukuza uchumi” alisema Satmah

Bidhaa za wajasiliamali kwenye banda la Halmashauri ya Wilaya ya Masasi

Satmah ameeleza kuwa Halmashauri imeendelea kupata ushindi wa kishindo mara tano Mfululizo, hivyo inaonesha jinsi watumishi wanavyojituma na kujitoa katika kuwatumikia wananchi kwa kufanya mambo kwa weledi, “nawapongeza kwa hilo maana wanaijengea Heshima halmashauri yangu”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Changwa Mkwazu alisema ushindi huo umetokana na kufanya kazi kwa ushirikiano lakini pamoja na kufanya kazi kwa kujituma sana hivyo ushindi huo unatupa deni la kujipanga zaidi katika maonesho yajayo ili kutetea ushindi huu tulioupata mara tano Mfululizo sasa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri  Changwa Mkwazu akipeana mkono wa Pongezi na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara mhe Gelasius Byakanwa  baada ya Halmashauri yake kupokea zawadi ya ushindi kwenye maonesho ya Nanenane 2018

Maonesho ya Nnanenane kwa mwaka 2018 yaliangazia katika kuongeza uzalishaji wa matumizi bora ya pembejeo na zana bora,uongezaji wa thamani ya Mazao kwa kufanya usindikaji na matumizi bora ya ardhi. 

 


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA MASASI DC 2025 January 14, 2025
  • MGAWANYO WA MAENEO YA UTAWALA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA TAREHE 27 NOVEMBA, 2024 MASASI DC September 18, 2024
  • MAENEO YA UTAWALA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI September 18, 2024
  • FURSA YA MIKOPO INAYOTOLEWA NA MFUKO WA MIKOPO KUTOKA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI November 12, 2021
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MASASI DC KWA KISHINDO:WATEMBELEA MIRADI MITANO YENYE THAMANI YA TSH.MILIONI 678,844,040.00

    May 19, 2025
  • WATENDAJI WA SERIKALI TEKELEZENI WAJIBU WENU WA KIKAZI,MSIJIHUSISHE NA MAMBO YA SIASA: BARAZA LA MADIWANI

    May 15, 2025
  • WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI NA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO ILI KUFANIKISHA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA AWAMU YA PILI.

    May 15, 2025
  • WATAALAMU MASASI DC WAPATIWA MAFUNZO YA MATUMIZI YA MFUMO WA UJIBUJI HOJA ZA CAG.

    May 11, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

KAIMU MKURUGENZI MASUMBUKO MTESIGWA AKABIZI OFISI KWA MKURUGENZI MPYA
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • RASIMU YA MPANGO WA BAJETI KWA MWAKA WA FWDHA 2021/2022 MASASI DC
  • Mpango Mkakati wa halmashauri ya wilaya ya masasi 2016/2017-2020/2021
  • Taarifa ya Hesabu ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2015/16
  • Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 Masasi DC
  • Uchunguzi wa Madai ya Korosho kwa Misimu ya 2016/17 NA 2017/18 Wilaya ya Masasi
  • Mpango Kzazi wa Manunuzi kwa mwaka wa Fedha 2017-2018 Masasi DC
  • Mwongozo wa Malalamiko
  • Sheria

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Mtwara Region
  • Hati ya Malipo (Salary Slip)
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya Ajira
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Masasi - Bomani

    Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi

    Simu ya mezani: 023-2510031

    Simu ya kiganjani: 023-2510031

    Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa