Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mkoaniMtwara imefanikiwa kununua gari lenye thamani ya shilingi milioni 89 kupitiafedha za mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2017/2018 lengo ikiwa ni kuboresha utoaji wa huduma pamoja na ukusanyaji wa mapato.
Akiongea wakati wa akipokea gari hilo,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mhe. Juma Satmahameipongeza menejimenti kwa kutekeleza mpango huo wa kununua gari kupitiamapato ya ndani kwani itasasidia kwa kiwango kikubwa ukusanyaji wa mapatoya ndani na hatimaye kuwezesha kutekeleza mipango mingine ya maendeleo.
Mhe. Satmah alisema kuwa “Kwa Halmashaurilazima tujipongeze kwa kuweza kukusanya mapato na kufanikiwa kununua garihili ambalo litawezesha halmashauri kutekeleza shughuli mbalimbali za kuhudumia wananchi ukizingatia halmashauri yetu ni kubwa hivyogari hili litasaidia kufikia maeneo mengi”
Ili halmashauri iweze kutekeleza shughulizake za kuhudumia wananchi ikiwemo utekelezaji wa miradi na huduma za jamiiikiwemo elimu,afya na maji inahitaji kuwa na fedha ambazo zinakusaywakwenye vyanzo mbalimbali vya ndani, hivyo Uwepo wa gari hilo utasaidiakurahisisha ukusanyaji wa mapato ili kutimiza malengo ya kuhudumia wananchi.
Halmashauri ya Wilaya ya Masasi imekuwana uungufu mkubwa wa magari baada ya kuunguiwa magari yake wakati wavurugu zilizotokea tarehe 26 Januari, 2013.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa