Asasi ya Haki Elimu imetoa msaada wa vitabu 823 kwa shule za msingi,sekondari na maktaba ya jamii wilayani masasi lengo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha elimu kwa kusaidia kuleta vitabu vya kufundishia na kujifunzia.
Aidha msaada huo umetolewa baada ya asasi hiyo kufanya tafiti katika shule hizo na kugundua kuwa moja ya changamoto katika sekta ya elimu ni ukosefu wa vitabu ambavyo ni nyenzo muhimu katika utoaji wa elimu bora kwa wananfunzi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vitabu hivyo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wialaya ya Masasi Bi Changwa Mkwazu, mwakilishi kutoka Hakielimu ndugu Ali Kamtambe alisema kuwa Hakielimu inafanya kazi na shule 4 ambazo zipo kwenye Mradi ikiwemo shule 2 kutoka Mpindimbi, Mtunungu na Isidori shirima ambapo shughuli mojawapo ni kuboresha elimu, pamoja na kuleta vitabu vya kujifunzia na kufundishia.
“Vitabu hivi vimethibitishwa ubora wake kwa matumizi ya kusomwa na wanafunzi na wananchi ni matumaini yetu kwamba vitabu hivi vitatumika kuboresha hali ya usomaji, taaluma na mwamko wa wananchi katika kupenda elimu” alisema Kamtambe.
Akipokea vitabu hivyo, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, aliishukuru asasi ya Hakielimu kwa kutoa msaada wa vitabu ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha elimu kwa wanafunzi lakini pia kwa jamii.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa