Mwenge wa uhuru 2024, jana tarehe 05/06/ 2024 umetembelea, kuona na kukagua mradi wa ujenzi wa ghala la kuhifadhia mazao la Maugura lililopo katika kijiji cha chiungutwa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, lenye uwezo wa kuhifadhi tani 10,000 za mazao pamoja na kutoa huduma za kijamii.
Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ilibuni mradi wa ujenzi wa ghala kwa kutumia mapato yake ya ndani kwa mwaka wa fedha 2021/2022, lengo likiwa ni kuongeza mapato yake ya ndani.
Aidha mradi huo, unatekelezwa na mkandarasi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na mkandarasi mdogo aliyeteuliwa Saleh Total Weighing Solution kwa mkataba wa shilingi 2,055,576,825.00 ambapo hadi sasa wakandarasi wamelipwa kiasi cha shilingi 928,222,240.17 kwa awamu tatu.
Kwa mujibu wa taarifa ya mradi huo iliyosomwa kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2024,mradi huu ulianza kutekelezwa rasmi tarehe 15/04/ 2022 na ulitarajiwa kukamilika tarehe 15/11/2022 lakini kutokana na ufinyu wa mapato ya ndani hivyo mradi huu sasa unatarajiwa kukamilika tarehe 30 june 2024.
Hata hivyo hatua za utekelezaji wa mradi huo kwa upande wa jengo la ghala ujenzi umekamilika kwa asilimia 90% na mkandarasi anaendelea na umaliziaji wa kupiga plasta eneo la nje, skimming kwenye ukuta, kupaka rangi na uwekaji wa sakafu ngumu (Niru).
Jengo la udhibiti ubora ujenzi umekamilika kwa asilimia 95% na mkandarasi anaendelea na ufungaji wa vifaa vya umeme, rangi na usafi wa jengo.
Na ujenzi wa mizani umekamilika kwa asilimia 99% ambapo inahusisha uagizwaji na ufungaji wa mzani mkubwa pamoja na ujenzi wa msingi wake, ujenzi wa ofisi ya mizani, ukamilishaji wa mfumo wa utoaji taarifa wa mzani usambazaji wa mzani wa tani 3, mzani mdogo wa 6 kg na kipima unyevu wa mazao.
Kazi iendelee!
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa