Halmashauri ya Enzkreis ya Nchini ujerumani yenye ushirikiano na Halmashauri za Masasi imekizawadia kituo cha mpira wa wavu cha mkalapa vifaa vya michezo (Mipira 10 na Neti 1) lengo kuboresha kituo hicho na kuwawezesha wachezaji kuendeleza vipaji vyao wakiwa shuleni
Akizungumza wakati wa kupokea mwalimu wa timu hiyo ndugu Gabriel Joshua alimweleza mwakilishi wa Enkreis ndugu Angela Gewiese kituo hicho kimeweza kutengeneza timu ya Mkoa ambayo ilishindana kitaifa katika Michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA na kuwa mshindi wa kwanza na wa pili kitaifa katika mchezo wa mpira wa wavu (volleyball)
“tunashukuru kwa msaada huu wa vifaa vya michezo maana vitasaidia timu kufanya mazoezi vizuri na hatimaye kuendeleza mchezo wa mpira wa wavu katika halmashauri yetu pamoja na kuendeleza vipaji wa wanafunzi ambavyo vitawasasidia katika maisha yao kwa kujiunga na vilabu vikubwa ndani na nje ya nchi” alisema Joshua.
Joshua alieleza kuwa, Ushindi huu umewapa nafasi wanafunzi walioshiriki michezo hii wamepata fursa ya kushiriki mashindano ya michezo Afrika mashariki “ni hatua nzuri kwa wanafunzi kuanza kutembelea nchi tofauti na kujifunza zaidi maana wataongeza ujuzi lakini pia kujifunza mambo mbalimbali kwa manufaa yao”
Kwa upande wake Mwakilishi wa Halmashauri ya Enzkreis ya Nchini Ujerumani Angela Gewiese alisema kuwa katika ushirikiano wao suala la elimu ni moja ya kipaumbele hivyo michezo ni sehemu ya kuboresha elimu kwa wananfunzi ndio maana baada ya kuona kituo hicho kifanya vizuri kwenye mchezo wa mpira wa wavu wameamua kukiwzesha vifaa vya mchezo huo.
Ushirikiano huo kati ya Masasi na Enzkreis ya Ujerumani ulianza mwaka 2011 ukilenga katika maeneo ya afya, mazingira, elimu, matumizi ya nishati jadidifu na mafunzo ya safari ambapo yanatekelezwa kwa lengo la kuboresha mazingira na utoaji wa huduma za afya ikiwemo uwekaji wa mifumo ya umeme jua kwenye zahanati 27 na nyumba 51 za watumishi wa Afya.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa