Mkuuu wa Kitengo Cha Fedha na uhasibu Halmashauri ya Wilaya Masasi Bw.Tumaini Mrango, amewaomba Watumishi wote wa Halmashauri hiyo kila mmoja kwa nafasi yake kuendelea kudumisha Umoja, ushirikiano, undugu na utendaji kazi wa pamoja ili Halmashauri iweze kufikia malengo yake.
Bw.Mrango ambaye Leo tarehe 29/09/2024 ni siku rasmi ambayo kwake anahitimisha Utumishi wa umma (anastaafu), katika barua yake maalumu aliyoiandika yakuwaaga timu ya Menejimenti Halmashauri ya Wilaya Masasi imesema kwamba anawashukuru wote kwa ushirikiano mkubwa ambao wamempatia katika Kipindi chote ambacho amekuwa nao wakati akihudumu kama Mkuu wa kitengo Cha Fedha na uhasibu.
"Nichukue fursa hii kuwaageni katika Utumishi wa umma nikiwa kama Mtumishi Mwandamizi na Mkuu wa kitengo Cha Fedha na uhasibu, nimekuwa nanyi tangu tarehe 13/04/2024 hadi leo tarehe 29,Septemba 2024 ni siku na tarehe yakuhitimisha Utumishi wangu, ninawashukuru wote ".
Bw.Mrango ameongeza kuwa kwake yeye Kama binadamu amewiwa kuwaaga na ana amini katika kutekeleza majukumu wapo waliotofautiana kwa njia moja ama nyingine, bali " mniwie radhi na niseme tu ilikuwa katika kutekeleza majukumu hali kadhalika kwa upande wangu moyo "u" safi ( nimesamehe yote). alisema Bw.Mrango
Hata hivyo Bw. Mrango amehitimisha maelezo katika barua yake kwa kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kuwaonyesha njia itakayo wapeleka kwenye mafanikio zaidi Watumishi hao kwa ukusanyaji, usimamizi na hasa katika kubuni vyanzo vipya vya mapato ambayo ndio moyo wa Halmashauri.
29/09/2024
@.. Masasi DC
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa