Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Mhe.Lauteri John Kanoni ameliagiza Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya Masasi kuunda haraka Sheria ndogo za Halmashauri zitakazodhibiti vitendo vya Wafugaji kuingiza mifugo yao kwenye mashamba ya Wakulima.
Kanoni ametoa agizo hilo Leo julai 30,2024 katika mkutano wa baraza la Madiwani la kupokea taarifa za kata, sanjali na kikao cha baraza la kawaida cha kupokea taarifa kutoka kwenye Kamati ambalo limefanyika Katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo Mbuyuni Masasi.
Amesema suala la migogoro ya Wafugaji na wakulima kwenye kikao kilichopita alitoa maelekezo kwamba, mwaka jana (2023 ) Serikali iliendesha oparesheni maalumu, na kwenye Wilaya yetu ya Masasi ilionekana suala hilo la migogoro ya Wafugaji na Wakulima ni himilivu halikuwa tishio kulinganisha na Wilaya zingine, "Lakini tuliagiza lazima Wafugaji na wakulima waishi kwa kuheshimiana na tukatoa maelekezo Kama kuna eneo kuna changamoto tupeni taarifa na tufanyie kazi"...alisema mhe.Kanoni
Ameongeza kuwa, suala hili la wakulima na Wafugaji lipo kwenye hatua ya udharura wake na wamekuwa wakipata taarifa kila siku na yeye kwa kushirikiana na vyombo vyake vya usalama baada ya kufuatilia changamoto waliyoibaini ya Kwanza ni wenyeviti wa vijiji wanapokea fedha kutoka kwa Wafugaji na wao wakishalisha mifugo yao katika eneo husika wanavamia katika maeneo mengine.
Aidha mhe.Kanoni ameendelea kuelezea kuwa, "tatizo Halmashauri yetu haina Sheria ndogo itakayotoa Mamlaka ya kudhibiti hilo hivyo nawapa kazi Mwenyekiti wa Halmashauri na baraza lako tengenezeni sheria ndogo na mniletee ili tumalize suala hili mara moja, sijashindwa mimi na Kamati yangu ya usalama, lakini pia tupate msaada kutoka kwa Wataalamu wa Halmashauri.
Hoja hiyo imeibuka mara baada ya Diwani wa Kata ya Mchauru mhe. Mussa Shaban kuelezea Moja ya changamoto kubwa inayowakabili wananchi wa kata hiyo ni Wafugaji kuvamia mashamba ya Wakulima na hatmaye hoja hiyo kuungwa mkono na waheshimiwa Madiwani ambao nao katika Kata zao changamoto ya mifugo kuingia katka mashamba ya Wakulima wanakumbana nayo.
Hata hivyo kuundwa kwa sheria ndogo za Halmashauri zitakazodhibiti vitendo vya Wafugaji kuingiza mifugo kwenye mashamba ya Wakulima inategemewa kuwa ni mwarobaini wa tatizo hilo ambapo sheria hizo zitatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.
@... Masasi DC
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa