DC KANONI: HONGERENI BARAZA LA MADIWANI KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO.
Mkuu wa Wilaya ya Masasi mhe.Lauter John Kanoni amempongeza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Masasi Ndg.Ibrahimu Chiputula, Madiwani wote, Pamoja na Wataalamu kwa kusimamia vizuri miradi ya Maendeleo ambayo inatekelezwa katika Maeneo Yao hususani ujenzi wa ghala la kuhifadhia Mazao lenye uwezo wa kupokea zaidi ya Tani elfu kumi (10,000/=) ambalo limejengwa Katika Kijiji Cha Chiungutwa, Kata ya Chiungutwa -Masasi.
Amesema kupitia ziara ya hivi karibuni iliyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara mhe.Luteni Kanali Patrick Kenani Sawala ya kukagua na kutembelea miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo na ikitarajiwa kufikiwa na mbio za Mwenge wa uhuru ifikapo june 05/2024, ameonyesha kuridhishwa na utekelezaji wa ujenzi huo wa ghala la kuhifadhia Mazao ambalo linajengwa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri linalogharimu kiasi Cha Fedha shilingi bilioni 1.8
Amesema "pamoja na uwepo wa changamoto mbalimbali za utekelezaji katika mradi ikiwemo shida ya umeme Lakini wote kwa ushirikiano wenu mliweza kuzitatua na hatmaye kuendelea na ujenzi ambao kwasasa upo katika hatua za mwisho za umaliziaji na ni ghala kubwa la mfano ambalo litaweza kuingiza mapato makubwa Ndani ya Halmashauri hii kwakwelii hongereni sana".........alisema
Mhe.Kanoni ametoa pongezi hizo Jana Tarehe 21/05/2024 katika mkutano wa baraza la Madiwani la kupokea taarifa za Shughuli za maendeleo Za kata, Pamoja na kujadili taarifa mbalimbali za Kamati.
Masasi DC...
Kazi iendeleeee!....
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa