Kanisa la Anglikani Dayosisi ya Masasi imetoa msaada wa vifaa vya shule kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu na wanaotoka kwenye mazingira magumu,akikabizi msaada huo padre Linus Buriani mbele ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi akiwa na Timu yake ya wakuu wa Idara mbalimbali,Msaada huo ni pamoja na Daftari zipatazo elfu mbili, Peni za wino zipatazo Elfu mbili na miatano,penseli zipatazo Mia sita, pamoja na Vifutio vya penseli Elfu moja. Vifaa hivyo vimegharimu kiasi cha shilingi 2,600,000.Baada ya kupokea msaada huo Mkurugenzi alitoa neno la shukurani na kusema“Napenda niwashukuru sana Dayosisi ya masasi kanisa la Anglikani kwa moyo wenu mulio uonyesha kwa kuwakumbuka na kuwajari watoto hawa wanaoishi kwenye mazingira magumu,hakika nyinyi ni mfano mzuri wa kuigwa, na nipende kuziasa Taasisi nyingine za kidini ziige kutoka kwenu na kuwa na moyo wa kutoa zaidi.” Hata hivyo kuna zaidi ya wanafunzi miamoja kutoka shule mbalimbali za msingi watanufaika na msaada huo.
Afisa Elimu Msingi kushoto akiwa pamoja na Afisa Maendeleo ya jamii kwa pamoja wakipokea shehena ya msaada wa vifaa vya shule kwa watoto wenye mahitaji maalumu
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa