Uongozi wa Shule ya Sekondari ya Chikoropola iliyopo Wilayani Masasi umeishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya Elimu nchini, ikiwemo ya Kata ya Chikoropola katika Shule ya Sekondari.
Aidha, taasisi hiyo imehaidi kuendelea kuunga mkono jitihada zote za maendeleo kwa kufanya kazi kwa juhudi, maarifa na uzalendo wa hali ya juu.
Mwalimu Daniel James Nyanda ni katibu wa Kamati ya ujenzi Shule ya Sekondari Chikoropola, amesema hayo Jana tarehe 06/05/2024 wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa umaliziaji wa Maabara ya Kemia katika Shule ya Sekondari Chikoropola mbele ya Kamati ya fedha ya Halmashauri ya Wilaya Masasi mara baada ya kutembelea na kukagua mradi huo.
Amesema Shule ya Sekondari Chikoropola ilipokea fedha (mapato ya ndani) kwa awamu mbili kwaajili ya umaliziaji wa ujenzi wa Maabara ya Kemia, ambapo awamu ya Kwanza ilikuwa ni tarehe 01/07/2023 na kiasi kilichopokelewa kilikuwa ni shilingi milioni 15 (15,000,000/,= na awamu ya pili ilikuwa ni tarehe 01/03/2024 na fedha iliyopokelewa ilikuwa ni shilingi milioni 15 (15,000,000/,= ), juma ni milioni 30 (30,000,000/=).
Ameongeza kuwa Shughuli za umaliziaji wa mradi zilianza rasmi Mwezi Disemba 2023 na mpaka Sasa mradi upo kwenye hatua za mwisho kabisa kukamilika kwani ujenzi umefikia takribani asilimia 95/%, na Shughuli zingine zinazoendelea ni kuweka tanki na kuunganisha mfumo wa Maji Safi katika Maabara, kumalizia ufunikaji wa mitaro katika Maabara, kujenga chemba ya mitungi ya gesi nyuma ya Maabara, kukamilisha ufungaji wa mfumo wa gesi, utengenezaji wa stuli 40 kwaajili ya Maabara, utengenezaji wa meza na kiti Cha Mwalimu kwenye chumba Cha Maabara na utengenezaji wa kabati la kuhifadhia vifaa vya Maabara na kemikali ndani ya chumba Cha maandalizi.
Nayo Kamati ya fedha ya Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Masasi pamoja na kuonyesha kuridhishwa na hali ya utekelezaji wa umaliziaji wa mradi huo, pia imeielekeza Kamati ya ujenzi kukamilisha kwa wakati Shughuli hizo ambazo zimesalia ifikapo tarehe 30/05/2024, na kama watabakiwa na pesa basi Halmashauri haitasita kuwaletea fedha zingine kuongeza kwaajili ya kuendelea kukamilisha mabaara zingine kama vile Maabara ya Bailojia, na Fizikia.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa