Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Bi.Mariam Kasembe amewataka Viongozi wa vyama vya Msingi AMCOS kutoa ushirikiano kwa Maafisa Ushirika ambao kimsingi ndio wanaotekeleza ilani ya CCM.
Amesema viongozi wengi wanaochaguliwa ndani ya AMCOS hizo wanajisahau na vyeo hivyo na kutowatambua kabisa Maafisa Ushirika, waheshimiwa Madiwani, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi na hasa pale wanapotaka Kujua kinachoendelea kwenye AMCOS zao.
Amesema "Ushirika upo kwenye ilani ya CCM, mnapotekeleza inamaana mnatekeleza ilani hiyo, na Ushirika ni mkusanyiko wa watu walioaminiana wakaunda chombo hicho ambacho ni cha Wananchi wenyewe sasa shida inakuja hawa viongozi wanaochaguliwa ndani ya AMCOS hizi hawawatambui wale Maafisa Ushirika, viongozi hawa hawataki hata Madiwani Kujua kinachoendelea kwenye AMCOS, hata Chama hawakitambui"... alisema Bi.Kasembe
Hata hivyo amewasisitizia watambue kuwa wapo katika nafasi hizo kwa ajili ya kutekeleza ilani ya CCM na matumaini yao ni kuona ushirika uwe na tija kwa wale watu wenyewe waliounda ushirika huo tofauti na hali ya sasa kwasababu malalamiko yamekuwa ni mengi yanayofikishwa katika Ofisi za Chama yakidai viongozi wa AMCOS kuwa ni vikwazo kwa wenye Ushirika huo kwani mara nyingi wamekuwa hawatendewi haki.
Aidha, Bi Kasembe amehitimisha kwa kuwakumbusha viongozi wa AMCOS wanapotekeleza majukumu yao wafuate kanuni na taratibu za Ushirika na kwamba Kila mmoja kwa nafasi yake atambue kuwa nyuma yake kuna watu wanataka awatimikie.
Na: Winifrida Ndunguru
..@..Masasi DC
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa