Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya Masasi limempongeza Mkuu wa Wilaya ya Masasi mhe.Lauter John Kanoni kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya ndani ya Halmashauri ya Wilaya Masasi.
Pongezi hizo zimetolewa leo tarehe 05/11/2024 na baraza hilo kwenye mkutano wa baraza la Madiwani la kupokea taarifa za kata (WDC) na mkutano wa baraza la kawaida ambao umefanyikia katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo uliopo mbuyuni Masasi.
Mhe.Ibrahimu Chiputula ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ametoa pongezi hizo kwa niaba ya baraza hilo amesema "mhe.Kanoni tunakupongeza kwa kazi kubwa na nzito ambayo unaifanya ndani ya Wilaya yetu mimi ninajivunia sana hata nikiwa Mkoani (Mtwara) huwa na sema mara kadhaa kuanzia Mkuu wa Mkoa hadi mkuu wa Wilaya wetu kazi kubwa wanazozifanya wanafanya kazi kubwa kwa vitendo, hadi tumeanza kumuita mzee wa matokeo"
Ameendelea kwa kusema kuwa "na mhe.mkuu wa Wilaya wetu toka afike hapa hakuna vitongoji Wala vijiji ambavyo hajawahi fika na anafanya kazi zaidi ya vijana, tumepambana kwenye mambo mengi na mhe.mkuu wa Wilaya mimi ninakushukuru sana na kama sio jitihada zake mambo mengine yasingeweza kupatikana mathalani hata katika usimamizi wa uingizwaji mizigo kwenye ghala letu la Halmashauri ambalo linapatikana katika Jimbo la lulindi na kuangalia changamoto zinazopatikna na kuona namna bora Halmashauri inaweza kuongeza mapato, mimi nikupongeze na kukushukuru sana.
05/11/2024
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa