Mkuu wa wilaya Masasi Ndugu. Selemani Mzee kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa ambaye alitarajiwa kuwa Mgeni Rasmi kwenye kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika leo cha kupitia hoja za CAG. Wakati akitoa salamu na Maagizo ya Mkuu huyo wa Mkoa selemani alisema "Nisingependa kupoteza muda wenu ila kwa niaba ya mkuu wa mkoa kwanza kabisa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya Masasi kwa kupata Hati Safi, na kutoa Maagizo yafuatayo,1.Kwenye vikao vijavyo ni vema Halmashauri ikamualika Mkaguzi na Mdhibiti mkuu wa serikali .Amewataka watumishi waache Uhodari wa kujibu hoja, badala yake wawe mahodari wa kupunguza Hoja na kuhakikisha majibu sahihi ya Hoja hizo yanapatikana ,.Ameitaka Halmashauri ya Masasi kupanua wigo wa vyanzo mbalimbali vya Mapato ya ndani ili kupunguza utegemezi kutoka serikali kuu pia ameitaka Halmashauri iweke Mpango madhubuti wa kununua Mashine za kukusanyia Mapato Pos ili kuongeza wigo wa Mapato,Lakini pia Mwisho kabisa aliitaka Halmashauri ya Wilaya kufanya Maandalizi ya mapema ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019.
Waheshimiwa Madiwani wa Kutoka kata mbalimbali Ndani ya Halmashauri ya Wilaya mapema leo 22/08/2019 wakiwa kwenye kikao maalumu cha kujadili Hoja Mbalimbali za ukaguzi za Hesabu za Halmashauri ya Wilaya masasi zinazoishia 30/06/2018 zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/2018Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya Masasi Ndugu.Saidi Lyuhuka akiwasilisha Hoja mbalimbali mbele ya waheshimiwa Madiwani, Timu ya ukaguzi ya Mkoa, pamoja na Mgeni rasmi na wakuu wa Idara na Vitengo kwa ajili ya majadiliano.
Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali wakisikiliza na kufuatilia kwa Makini Hoja mbalimbali zinazohusu Idara zao wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani lilofanyika mapema leo 22/08/2019
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa