• Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Masasi District Council
Masasi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Asili ya Masasi
      • Historia ya Masasi Kiutawala
      • Orodha ya Viongozi
      • Ukubwa wa eneo
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi wa Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Ugavi na Ununuzi
      • Sheria na Usalama
      • Nyuki
      • Tehama na Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Agriculture
    • Construction Minerals
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Upimaji wa Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Utawala na Mipango
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
      • Elimu Afya na Maji
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • Jarida
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI LAVUNJWA RASMI.

Posted on: June 19th, 2025


Na.Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini(W) Masasi.


Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara leo tarehe 19/06/2025 limevunjwa rasmi huku wakimtaka Mkurugenzi Mtendaji Ndg.Alphaxad Etanga pamoja na Watendaji wake wote kuwa makini kwenye suala zima  la Mapato ili kufikia lengo la Halmashauri la kukusanya zaidi ya shilingi bilioni kumi kwa Mwaka.

Madiwani hao pia wamewataka watendaji na Wataalamu kwa ujumla kuhakikisha wanasimamia vizuri ile asilimia 10 ya mapato ya ndani waliyoipanga inapelekwa kwenye Miradi ya Afya.

Maagizo hayo yametolewa kwenye Mkutano maalumu wa Baraza la mwisho la Madiwani ambalo lilianza mnamo mwaka 2020 na kuhitimishwa leo juni 19,2025.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Ndg.Alphaxard Etanga akisoma taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Maendeleo katika kipindi cha Miaka mitano (2020/21 -2024/25) pamoja na mapendekezo ya uendeshaji wa shughuli za Halmashauri kipindi cha Mpito, amesema katika kipindi cha miaka 5 baraza limepata mafanikio makubwa ambapo jumla ya shule mpya saba (7) za msingi zimejengwa na kusajiliwa na kufanya jumla ya shule 137 kutoka shule 130 zilizokuwepo mwaka 2020/2021.

Amesema kwa hatua hiyo takwimu za uandikishaji wa darasa la awali zimepanda kutoka Wanafunzi 6395 hadi 6745 sawa na ongezeko la 5% huku elimu msingi uandikishaji umeongezeka kutoka 7835 hadi 8464 sawa na asilimia 8% ya uandikishaji.

"Kwa Sekta  ya elimu Sekondari shule za Serikali zimeongezeka kutoka shule 27 hadi kufikia shule 37 zenye usajili na hii ikiwa ni ongezeko la asilimia 10 na kufanya kila kata katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kuwa na shule za Sekondari,kwaiyo haya ni mafanikio makubwa yanayotokana na usimamizi wenu Madiwani " alisisitiza Ndg.Etanga

Akizungumzia sekta ya Afya Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa kwa kipindi cha Miaka mitano hali ya upatikanaji wa Dawa katika Hospitali ya Wilaya, Vituo vya afya na Zahanati imeongezeka kutoka asilimia 88% hadi 96% sawa na ongezeko la asilimia 8%.


"Kwa kiupekee nimshukuru sana Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha nyingi ambazo zimeleta tija kubwa kwa jamii ya wana Masasi Katika kipindi cha Miaka mitano "

Sambamba na hilo Halmashauri kwa kutambua mchango mkubwa walioutoa viongozi hao imetoa vyeti vya pongezi kwa Madiwani wa kata zote 34 pamoja na wabunge wa jimbo la Ndanda na Lulindi.


19/06/2025

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA MASASI DC 2025 January 14, 2025
  • MGAWANYO WA MAENEO YA UTAWALA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA TAREHE 27 NOVEMBA, 2024 MASASI DC September 18, 2024
  • MAENEO YA UTAWALA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI September 18, 2024
  • FURSA YA MIKOPO INAYOTOLEWA NA MFUKO WA MIKOPO KUTOKA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI November 12, 2021
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI LAVUNJWA RASMI.

    June 19, 2025
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA YAANZA VIZURI MASASI DC

    June 17, 2025
  • MSIGWA: MAAFISA HABARI NI SAUTI YA SERIKALI, TANGAZENI MAFANIKIO YA SERIKALI KWENYE MAENEO YENU.

    May 25, 2025
  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI MNAKUWA WABUNIFU NA WAZALENDO ILI WANANCHI WAPATE HABARI SAHIHI NA KWA WAKATI.

    May 23, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

KAIMU MKURUGENZI MASUMBUKO MTESIGWA AKABIZI OFISI KWA MKURUGENZI MPYA
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • RASIMU YA MPANGO WA BAJETI KWA MWAKA WA FWDHA 2021/2022 MASASI DC
  • Mpango Mkakati wa halmashauri ya wilaya ya masasi 2016/2017-2020/2021
  • Taarifa ya Hesabu ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2015/16
  • Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 Masasi DC
  • Uchunguzi wa Madai ya Korosho kwa Misimu ya 2016/17 NA 2017/18 Wilaya ya Masasi
  • Mpango Kzazi wa Manunuzi kwa mwaka wa Fedha 2017-2018 Masasi DC
  • Mwongozo wa Malalamiko
  • Sheria

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Mtwara Region
  • Hati ya Malipo (Salary Slip)
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya Ajira
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Masasi - Bomani

    Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi

    Simu ya mezani: 023-2510031

    Simu ya kiganjani: 023-2510031

    Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa