Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara imejadilili imepitisha mapendekezo ya rasimu ya mpango wa bajeti zaidi ya shilingi bilioni 34.4 kwa mwaka 2019/2020 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mapendekezo hayo yamepitishwa leo na Baraza la Madiwani katika Mkutano maalum wa kupitisha rasimu hiyo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
Akiwasilisha mapendekezo ya rasimu ya bajeti hiyo katika baraza la madiwani, Afisa Mipango wa Halmashauri ndugu Jeremiah Lubeleje kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Chwangwa Mkwazu, alisema kuwa lengo la Halmashauri ni kukusanya shilingi bilioni 34.4 ambapo kati za hizo zaidi ya shilingi bilioni 2.3 ni mapato ya ndani.
Kwa mapato ya ndani, Halmashauri itakusanya kupitia ushuru wa mazao kilimo, ushuru wa mazao ya misitu, ushuru wa huduma, madini ya ujenzi, leseni za biashara, ada za upimaji mashamba, stendi na vyanzo vingine
Lubeleje alifafanua kuwa kwenye matumizi mengineyo Halmashauri imepanga kutumia shilingi bilioni 1.02, kwa ajili ya miradi ya maendeleo jumla ya shilingi bilioni 4.3 kwa upande wa mishahara zaidi ya bilioni 26.7 zimepangwa kutumika kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Juma Satmah alisema kuwa kwa bajeti hiyo Halmashauri imeongeza vyanzo vya mapato ili kuoboresha utendaji kazi wa kuhudumia wananchi ikiwemo utekelezaji wa miradi ampao katika mwaka 2019/2020 hamashauri itatumia zaidi ya bilioni 1.1 kutoka atika mapato ya ndani kwa ajili ya kutekelezaji wa miradi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya shule.
Satmah aliongeza kuwa bajeti hiyo pia imelenga kuimarisha kuimarisha sekta ya kilimo mifugo na uvuvi ili kuboresha sekta hio ukizingatia sehemu kuwa ya mapato ya ndani ya halmashauri hiyo yanatokana na kilimo ambapo shilingi milioni 181,532,000 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa ghala la mazao pamoja na kuanzisha shamba darasa.
Aidha mwenyekiti amesema bajeti hiyo imezingatia kutoa mchango wa asilimia kumi (10%) wananwake na vijana kutoka mapato ya ndani.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa