• Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Masasi District Council
Masasi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Asili ya Masasi
      • Historia ya Masasi Kiutawala
      • Orodha ya Viongozi
      • Ukubwa wa eneo
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi wa Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Ugavi na Ununuzi
      • Sheria na Usalama
      • Nyuki
      • Tehama na Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Agriculture
    • Construction Minerals
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Upimaji wa Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Utawala na Mipango
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
      • Elimu Afya na Maji
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • Jarida
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI LAFIKIA UKOMO WA MADARAKA RASMI

Posted on: June 10th, 2020

Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Masasi limefika ukomo wake leo rasmi tarehe 10 Juni, 2020 tangu lilipoaanzishwa rasmi tarehe 10 Desemba, 2015.

Akizungumza kwenye Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani la kupokea taarifa ya ukomo wa madaraka ya waheshimiwa madiwani wa Halmashauri hiyo, Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Masasi Seleman Mzee amewapongeza madiwani kwa ushirikiano walioonesha katika kusimamia shughuli za maendeleo kadri walivyoweza katika kipindi chote cha uongozi wao.

Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Masasi Seleman Mzee (aliyesimama) akitoa nasahaa wakati wa mkutano maalumu wa ukomo wa maraka ya madiwani tarehe 10 juni,2020

Aidha amewatakia kila la heri kwa watakaoingia kwenye kinyang'anyilo cha udiwani katika uchaguzi ujao na kuwakumbusha kuzingatia taratibu, kanuni na sheria za uchaguzi ili kuepuka kuchukuliwa hatua.

Kwa upande wake mhe Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Juma Satmah amewaeleza wajumbe kuwa kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Halmashauri imefanikiwa kukusanya mapato ya ndani kwa asilimia 129.13 ambapo jumla shilingi 2,898,063,619.08 zimekusanywa kati ya shilingi 2,244,382,000 zilizokadiriwa kukusanywa. "Hii ni sawa na ongezeko la 29.13% tunastahili kujipongeza kwa mafanikio haya"


Satmah aliendelea kufafanua kwa  wajumbe kuwa Halmashauri imetekeleza miradi ya sekta mbalimbali kupitia vyanzo mbalimbali cha mapato mfano" kwa idara ya msingi tumefanikiwa kujenga vyumba vya madarasa 126, vyoo matundu 660, nyumba za Walimu 9 na madawati 1674"

Kwa upande wa sekondari, miundombinu ya mabweni ,madarasa 45 maabara 3 vyoo matundu 270, nyumba za watumishi 13 imejengwa pamoja na kutengeneza viti 980 na meza 904 lengo ikiwa ni kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia. Iadha kwa upande wa afya huduma zimeendelea kuboreshwa ambapo kwa kipindi cha miaka 5 tumefanikiwa kupanua vituo vya afya 3, ujenzi wa zahanati 7 pamoja na ujenzi wa hospitali ya Halmashauri eneo la Mbuyuni.  

mhe Mwenyekiti wa Halmashauri  Juma Satma akiwasilisha taarifa kwa Wajumbe kwenye mkutano maalumu  wa ukomo wa maraka ya madiwani tarehe 10 juni,2020

Aidha, Satmah amewapongeza wajumbe wa baraza hilo kwa ushirikiano walioonesha wakati wote wa uongozi wao pamoja na uvumilivu wa kufanya kazi bila kupata stahiki zao kwa muda wa Miesi 18 hali iliyosababishwa na upungufu wa mapato kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

"Ni vizuri kubuni vyanzo vipya vya mapato badala ya kutegemea ushuru wa korosho pekee ili tatizo kama hilo lisijitokeze tena kwa waheshimiwa madiwani watakaofanikiwa kurudi baada ya uchaguzi"

Nae Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Bibi Changwa Mkwazu amewashukuru waheshimiwa madiwani kwa ushirikiano walioonesha kwa kipindi chote cha uongozi wao kwani kwa pamoja wameweza kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo kwa wananchi ikiwemo usimamizi wa miradi ya maendeleo na matumizi ya fedha za serikali hali ilipelekea halmashauri kupata HATI safi katika kaguzi mbalimbali za hesabu za serikali.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA MASASI DC 2025 January 14, 2025
  • MGAWANYO WA MAENEO YA UTAWALA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA TAREHE 27 NOVEMBA, 2024 MASASI DC September 18, 2024
  • MAENEO YA UTAWALA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI September 18, 2024
  • FURSA YA MIKOPO INAYOTOLEWA NA MFUKO WA MIKOPO KUTOKA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI November 12, 2021
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • MSIGWA: MAAFISA HABARI NI SAUTI YA SERIKALI, TANGAZENI MAFANIKIO YA SERIKALI KWENYE MAENEO YENU.

    May 25, 2025
  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI MNAKUWA WABUNIFU NA WAZALENDO ILI WANANCHI WAPATE HABARI SAHIHI NA KWA WAKATI.

    May 23, 2025
  • MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MASASI DC KWA KISHINDO:WATEMBELEA MIRADI MITANO YENYE THAMANI YA TSH.MILIONI 678,844,040.00

    May 19, 2025
  • WATENDAJI WA SERIKALI TEKELEZENI WAJIBU WENU WA KIKAZI,MSIJIHUSISHE NA MAMBO YA SIASA: BARAZA LA MADIWANI

    May 15, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

KAIMU MKURUGENZI MASUMBUKO MTESIGWA AKABIZI OFISI KWA MKURUGENZI MPYA
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • RASIMU YA MPANGO WA BAJETI KWA MWAKA WA FWDHA 2021/2022 MASASI DC
  • Mpango Mkakati wa halmashauri ya wilaya ya masasi 2016/2017-2020/2021
  • Taarifa ya Hesabu ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2015/16
  • Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 Masasi DC
  • Uchunguzi wa Madai ya Korosho kwa Misimu ya 2016/17 NA 2017/18 Wilaya ya Masasi
  • Mpango Kzazi wa Manunuzi kwa mwaka wa Fedha 2017-2018 Masasi DC
  • Mwongozo wa Malalamiko
  • Sheria

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Mtwara Region
  • Hati ya Malipo (Salary Slip)
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya Ajira
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Masasi - Bomani

    Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi

    Simu ya mezani: 023-2510031

    Simu ya kiganjani: 023-2510031

    Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa