BARABARA YA NDANDA- MIYUYU YENYE UREFU WA KM 0.8 KWA KIWANGO CHA LAMI YATEMBELEWA NA MWENGE WA UHURU 2024.
Mwenge wa uhuru kitaifa 2024, umetembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Barabara ya Ndanda-Miyuyu yenye urefu wa km 0.8 kwa kiwango cha lami na upana wa mita 8.0
Mradi huo ambao umefanywa na mkandarasi M.R Building & Civil Engineering Co.Ltd katika mwaka wa fedha 2023/24 chini ya usimamizi wa Ofisi ya Meneja wa TARURA Wilaya ya Masasi ulianza utekelezaji wake tarehe 19/09/2023 na umekamilika tarehe 15/5/2024 kwa mujibu wa mkataba wake.
Kazi zilizofanyika mpaka sasa ni ujenzi wa barabara ya lami (0.8) na upana mita 8,ujenzi wa kalavati-1 na ujenzi wa mifereji kwa kutumia mawe mita za mraba 3,310.35
Kulingana na taarifa ya mradi ni kwamba manufaa ya mradi huo ni pamoja na kupungua kwa gharama za matengenezo zilizokuwa zikitumika kila mwaka, kurahisisha usafiri kwa wananchi kufika hospitali ya rufaa Ndanda, kupunguza ajali za barabarani kwa kiwango kikubwa na ajira kwa vikundi maalumu wakati wa ujenzi wakiwemo akina mama, mama lishe na vijana.
Aidha, gharama za utekelezaji wa mradi ni shilingi 444,108,727.27 zikiwa ni fedha za maendeleo mfuko wa jimbo kutoka hazina kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024. Hadi sasa mkandarasi amelipwa tsh 303,609,636.36 sawa na asilimia 68.36
Kazi iendelee!
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa