Leo tarehe 11.12. 2018 Balozi wa Japani nchini Tanzania mhe.Shinichi Goto, amekabidhi madarasa 7, Madawati 65 na vyoo matundu 12 kwa shule za Msingi Nakachindu na Chipango yenye thamani ya shilingi 210,791,600 yaliyojengwa kwa usimamizi wa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Life Improvement Association (TALIA).
Madarasa 4 katika shule ya msingi Nakachindu yaliyojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan
Akiongea wakati wa kuzindua na kukabidhi miundombinu hiyo kwa Uungozi wa Wilaya na shule hizo, Balozi Shinichi Goto alisema kuwa nalishukuru shirika la TALIA kwa usimamizi mzuri kwani majengo yamejengwa kwa viwango vizuri kama ilivyokusudiwa.
Balozi Shinichi Goto amesema “tunaishukuru TALIA kwa kusimamia vizuri wa miradi hii hadi kukamilika na leo tunakabidhi kwa Halmashauri tayari kwa matumizi, tunaamini imesaidia kutatua tatizo la upungufu wa madarasa, vyoo na madawati kwa shule hizi na hivyo wanafunzi watakuwa na mazingira bora ya kujifunzia”
Balozi wa Japani nchini Tanzania mhe.Shinichi Goto ( aliyeshika mike) akisoma tarifa wakati wa hafla ya kukabidhi miundombinu katika shule ya Msingi Nakachindu
Aidha Balozi Shinichi Goto ameeleza kuwa, Japani itaendelea kutoa Misaada ya kimaendeleo Halmashauri ya Wilaya ya Masasi na Tanzania kwa ujumla kama sehemu ya kuimarisha uhusiano kati ya Nchi ya Tanzania na Japani.
Akisoma taarifa ya hali ya Miundombinu ya Shule za Msingi ya Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kwa Balozi wa japani nchini Tanzania Mhe. Shinichi Goto Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Selemani Mzee ameeleza kuwa, Halmashauri inaupungufu wa vyumba vya madarasa 777 kati ya 1579 yanayohitajika, hivyo ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa umetatua changamoto ya upungufu wa madarasa na vyoo katika shue hizi mbili ambpo kwa sasa hakuna uungufu kabisa.
Mkuu wa Wilaya amemweleza Balozi Shinichi Goto kuwa “kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha Nakachindu na Chipango napenda kutoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Japan kupitia shirika lisilo la kiserikali la TALIA kwa msaada huu mkubwa wa ujenzi wa vyumba 4 vya madarasa, matundu ya vyoo 12 na madawati 44 kwa shule ya msingi Nakachindu na vyumba 3 na madawati 17 kwa shule ya msingi Chipango kwani shule hizi hazina upungufu tena wa miundombinu hii”.
Madarasa 3 katika shule ya msingi Chipango yaliyojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan
Kwa uande wake Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Bibi Changwa Mkwazu, ameahidi kuitunza miundombinu hiyo ili idumu kwa kipindi kirefu kwani ni kigezo kikubwa cha kuongeza ari ya wanafunzi kuwa na mazingira mazuri ya kujifunza na kujifunzia ambalo ndilo lengo a serikali katika kuboresha elimu.
Akiongea kwa niaba ya wananchi wa Nakachindu bibi Asha Said ameshukuru msaada huo wa miundombinu kwani awali shule hiyo ilikuwa na vyumba vitatu tu vya madarasa hai iliyokuwa inapelekea wanafunzi wa madarasa tofauti kutumia chumba kimoja cha dara kusoma, ilikuwa ngumu sio tu kwa wanafunzi hata walimu na ilikuwa inachangia kwa kiasi kikubwa wanafunzi wengi kutofanya vizuri katika masomo yao.
Mkuu wa wilaya ya masasi mhe. selemani Mzee (wa kwanza kulia) akikabidhi taarifa kwa Balozi wa Japani nchini Tanzania mhe.Shinichi Goto
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa