Mahakama ya hakimu Mkazi ya Wilaya ya Masasi, katika Mkoa wa Mtwara imemuhukumu Ally Musa Katambo (30) wa kata ya Chikundi Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wake wa miaka 11.
Hukumu hiyo ilitolewa leo na Hakimu Mkazi Honorious Kando alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo julai 7, Mwaka jana nyumbani kwake.
Kando alieleza kuwa kwa mujibu wa maelezo ya mshitakiwa , alikili kutenda kosa hilo kutokana na ugumu wa maisha ndipo akaamua kwa mganga wa kienyeji ambaye alimshauri kuwa ii apate utajiri afanye mapenzi na ndugu yake wa damu ndipo alipomshawishi mtoto wake wa miaka 11 na akafanya nae mapenzi ili awe tajiri.
“Ili iwe fundisho kwa mshitakiwa mwenyewe na jamii kwa ujumla, mshitakiwa utaenda jela miaka 30” alisema Hakimu Kando.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Kando alisema kuwa kwa mujibu wa uchunguzi wa Daktari mtoto alipata madhara katika viungo vyake vya uzazi ambapo alipatwa na maumivu makali ya tumbo hali iliyopelekea akafanyiwa upasuaji kwenye via vyake vya uzazi ili kuondoa uvimbe uliosababishwa na kubakwa mara nyingi na baba yake mzazi.
Kwa upande wake Baba Mzazi wa mtuhumiwa bwana Musa Katambo alipoulizwa na Hakimu kwanini alikuwa anazimia wakati anapomtembelea mjukuu wake Hospitali, aliieleza Mahakama kuwa ilikuwa ni kwa sababu jambo hilo hajawahi kulishuhudia tangu amezaliwa na hivyo yuko radhi sheria ichukue mkondo wake.
Kwa mujibu wa mwendesha mashitaka Inspeta Koplo Selemani aliieleza Mahakama kuwa kutokana na kosa alilolifanya mtuhumiwa ni vema apewe adhabu kali ili fundisho kwa wengine katika jamii.
Pia Mwendesha mashitaka Inspeta Koplo Selemani aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo akitambua kuwa huyo ni mtoto wake wa kumzaa aliweza kumbaka na kutenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 158 (1)(2) Sheria ya kanuni ya adhabu (Penal Code) Namba 16 kama ilivyoboreshwa mwaka 2002.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa