Mkuu wa Wilaya ya Masasi mhe.Lauter Kanoni amewaomba Waheshimiwa Madiwani kuendelea kuwahamasisha Wananchi wajitokeze kupiga kura ifikapo Nov 27, 2024 ili kuwachagua viongozi muhimu wa Serikali za Mitaa wanaowataka.
Mhe.kanoni ametoa ombi hilo Katika baraza la kawaida la Madiwani ambalo limefanyika Jana tarehe 05/11/2024 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri uliopo mbuyuni Masasi, ambapo amesema kwamba katika zoezi la uandikishaji kwa Halmashauri ya Wilaya Masasi takwimu inayoonyesha Wananchi wamejitokeza kwa wingi sana Sawa na asilimia 85 "hongereni sana, hivyo tunaomba Tarehe 27/11/2024 kama walivyojitokeza kwenye kujiandikisha basi waende wakapige kura na kuwachagua viongozi Bora wanaowataka."
Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Masasi mhe.Ibrahimu Chiputula ameongeza kuwa katika suala hilo la uchaguzi wao waheshimiwa Madiwani wanayo nafasi kubwa na Jamii inawaamini hivyo kila mmoja kwa nafasi yake kwenye eneo lake "tukashiriki kwenye jambo la kuwahimiza Wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura tarehe 27/11/2024, tukaiongeze hiyo Kasi sasa kwenye kupiga kura."
Pia mhe.Chiputula amehitimisha kwa kuwaomba Watendaji wa Serikali wajiepushe na Mambo ya Siasa kuwa na ushabiki na Chama cha chochote Cha Siasa, bali wanatakiwa wasimame kwa nafasi Yao ya utendaji ili kuepuka kuvuruga Zoezi hilo la uchaguzi.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika Nov 27,2024 huku nafasi mbalimbali zitapigiwa kura ikiwemo nafasi ya Mwenyekiti wa Kijiji, Mwenyekiti wa kitongoji, Wajumbe wa Halmashauri ya vijiji na wajumbe Halmashauri ya Vijiji kundi mchanganyiko la Wanawake.
serikalizamitaasautiyawananchijitokezekushirikiuchaguzi.
06/11/2024
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa