Halmashauri ya wilaya ya masasi kupitia idara ya maendeleo ya jamii imesajili vikundi vya kiuchumi vyenye idadi ya 1137.
Halmashauri ya wilaya ya Masasi kupitia idara ya maendeleo ya jamii imejiwekea utaratibu wa kuvipa ujuzi vikundi vya kijamii na kiuchumi
Ufuatao ni utaratibu wa kuandikisha kikundi .
Kikundi cha kiuchumi na kijamii lazima kiwe na rasimu katiba iliyoandaliwa na wanakikundi wote.
Rasimu hiyo ikishakuwa tayari huwasilishwa kwa Afisa Maendeleo ya jamii kwaajili ya ushauri wa kitaalamu.
Baada ya rasimu kupitiwa na kukubalika na wanakikundi wote, rasimu huthibitishwa kuwa katiba rasmi ya kikundi.
Baada ya katiba kukamilika, kikundi husika huketi na kuandaa muhtasari ambao ndani yake unakuwa na agenda kuu ya kuomba kuandikishwa kwa Mkurugenzi Mtendaji (W) kwani katika halmashauri ndiye mwenye mamlaka ya kuidhinisha mamlaka ya kuidhinisha kuandikisha kikundi.
Muhtasari huo huambatishwa na barua ya kuomba kuandikishwa ambayo inapitishwa na kusainiwa kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtendaji wa Kata.
Mkurugenzi akishatoa idhini ya kikundi husika kuandikishwa, kikundi kina wajibu wa kulipia Tshs 20,000 elfu ishirini tu ikiwa ni gharama za uandikishaji.
Fedha za uandikishaji zinalipiwa benki kupitia akaunti ya halmashauri, ambapo pay in slip iliyotoka benki huwasilishwa ofisi ya uhasibu na kukatiwa risiti ya kielektroniki ya kukiri mapokezi ya fedha.
Kikundi kinaandikishwa katika daftari la kudumu la halmashauri na kupatiwa namba rasmi inayotambulika.
Kikundi kinapatiwa cheti cha uandikishaji kinachosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji pamoja na Afisa Maendeleo ya ndani.