• Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Masasi District Council
Masasi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Asili ya Masasi
      • Historia ya Masasi Kiutawala
      • Orodha ya Viongozi
      • Ukubwa wa eneo
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi wa Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Ugavi na Ununuzi
      • Sheria na Usalama
      • Nyuki
      • Tehama na Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Agriculture
    • Construction Minerals
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Upimaji wa Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Utawala na Mipango
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
      • Elimu Afya na Maji
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • Jarida
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Kujua Ufugaji bora wa kuku

KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU

 

Watu wengi hujihusisha na ufugaji wa kuku kwa lengo la kujipatia chakula na kipato. Mazao yatokanayo na ufugaji wa kuku ni pamoja na mayai, nyama, mbolea na manyoya kwa matumizi mbalimbali. Mifumo ya ufugaji kuku ambayo hutumika hapa nchini ni huria, nusu huria na shadidi. Ufugaji wa kuku utakuwa endelevu na wenye tija kwa kufuata kanuni za ufugaji bora zifuatazo:-

 

  • Kufuga kuku kwenye banda bora,
  • Kuchagua kuku bora wa kufuga,
  •  Kutunza na kulisha kuku kulingana na hatua mbalimbali za ukuaji
  • Kudhibiti na kutibu magonjwa ya kuku;
  • Kutunza kumbukumbu.

 


1 Banda la Kuku

 

Kuku huhitaji banda bora ili wasiathirike na madhara mbalimbali. Banda

 

bora la kuku linatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-

 
  • Imara, lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya na pia dhidi ya hali ya hewa hatarishi kwa mfano jua kali, upepo, baridi na mvua pamoja na wanyama hatari,
  • Lenye mwanga, hewa na nafasi ya kutosha inayoruhusu usafi kufanyika kwa urahisi,
  • Lijengwe sehemu yenye mwinuko isiyotuama maji, isiyo na upepo mkali na iwe mbali kidogo na nyumba ya kuishi watu,
  • Liwe na vichanja kwa ajili ya kuku kupumzika na kulala
  • Liwe na sehemu ya kuwekea chakula, maji, kutagia, kuatamia na sehemu ya kulelea vifaranga,
  • Liwe na nafasi ya kutosha kulingana na idadi ya kuku na kuweka vyombo vya chakula na maji,
  • Kwenye mazingira ya joto banda liwe la ukuta mfupi na sehemu ya kubwa wazi yenye wavu hadi kufikia kwenye paa;
  • Kwenye mazingira ya baridi banda liwe na ukuta mrefu unaokaribia paa na sehemu ndogo tu iwe wazi yenye wavu ili kupitishia hewa na mwanga.
 

1.1 Vifaa Vinavyotumika kwa Ujenzi wa Banda

 

Vifaa vya kujengea banda vizingatie gharama na upatikanaji wake katika eneo husika. Baadhi ya vifaa hivyo ni kama ifuatavyo:-

 
  • Sakafu - Saruji, udongo, mbao, mianzi au fito
  • Kuta - Fito, mabanzi, mbao, nguzo mianzi, udongo, matofali,
  • mawe, mabati na wavu
  • Paa - Nyasi, makuti, majani ya migomba, mabati na vigae.
  • Wigo - Matofali, mbao, fito nguzo, mabanzi, mianzi,matete,
  • wavu na mabati
 

1.2 Ukubwa wa Banda

 

Ukubwa wa banda utategemea idadi ya kuku na aina ya kundi la kuku. Kuku wanahitaji nafasi tofauti kutegemea umri, aina na njia ya ufugaji. Eneo la mita moja ya mraba linatosha kwa vifaranga 16 wa umri wa wiki 1 – 4. Hivyo banda lenye mita za mradi 16 linaweza kulea vifaranga 320 hadi wiki 4. Baada ya wiki 4 eneo hili liongezwe kutegemea aina ya kuku na njia inayotumika katika ufugaji kama inavyoonekana kwenye jedwali Na. 1

   

Jedwali Na. 1.  Eneo Linalohitajika Kufuga Kuku Kwenye Sakafu ya Matandazo

 

  Kutegemea na Umri na Aina ya Kuku

 
Umri wa kuku
Idadi ya kuku kwa mita moja ya mraba
 
Kuku wa Mayai
Kuku wa Nyama
Siku 1 hadi wiki 4

18

18

Wiki ya 5 hadi 8

9

9

Wiki ya 9 hadi 20

6

0

Wiki 21 kuendelea

3-4

0

 

 

 

Angalizo:

 

Mabanda yanayozungushiwa wigo kama ilivyo katika mfumo wa nusu huria, kuku mmoja huhitaji eneo la wazi lenye ukubwa wa mita za mraba 10. Mfano, kuku 100 huhitaji eneo la mita za mraba 1000

  

1.3 Vifaa na Vyombo Muhimu

 

Mfugaji anashauriwa kutumia vifaa na vyombo maalum ili kurahisisha na kuboresha utunzaji wa makundi mbalimbali ya kuku. Vifaa na vyombo vinavyohitajika kwa ajili ya kuwekea chakula na maji, kutagia mayai na kupumzika vinapatikana kwenye maduka ya pembejeo za mifugo. Aidha, mfugaji anaweza kutengeneza mwenyewe kwa kutumia malighafi zilizopo kwenye mazingira yake.

  

2 Uchaguzi wa Kuku Bora wa Kufuga

 

2.1 Kuku wa Asili

 

Aina za kuku wa asili wanaopatikana hapa nchini ni pamaja na Kuchi (Kuza), pori (Kishingo), Njachama, Kinyavu, Mbuni na Tongwe (Msumbiji). Mfugaji anaweza kuongeza uzalishaji kwa kuchagua kuku mwenye sifa zifuatazo:-

 
  • Uwezo wa kutaga mayai mengi (kati ya 15-200 katika mzunguko
  • mmoja wa utagaji (Jedwali Na 2),
  • Uwezo wa kuatamia na kuangua vifaranga wengi,
  • Uwezo wa kustahimili magonjwa
  • Umbo kubwa na kukua haraka.
      

Jedwali Na. 2.  Masuala ya Kuzingatia Wakati wa Kumchagua Kuku

 

       Mtagaji Asili

 
Viungo vya Mwili
Sifa
Macho
Maangavu, yenye wekundu kwa mbali na
makubwa yamejaa kwenye soketi za
macho.
Mdomo
Wenye rangi ya njano kwa mbali
Kisunzu/Upanga
Chekundu, Laini,kimelala kidogo upande
na kinang’aa
Shingo
Iliyosimama
Umbali kati ya kidali
na nyonga
Upanga wa vidole 3-4 vya mpimaji
Upanga wa nyonga
Upana wa vidole 3 vya mpimaji
 

2.2 Kuku wa Kisasa

 

Kuku bora wa kisasa kwa ajili ya mayai au nyama ni mwenye sifa

 

zifuatazo:-

 
  • Uwezo wa kuanza kutaga wakiwa na umri mdogo (miezi 5-6)
  • kutegemea na koo,
  • Umbo kubwa na anayekula haraka (kilo 1.5-2.0 kwa kipindi cha
  • wiki 8-120 kutegemea na koo kwa kuku wa nyama,
  •  Anayetaga mayai mengi (250 au zaidi) kwa kuku wa mayai kwa
  • mwaka; na
  • Awe na uwezo wa kutaga katika umri wa miezi 6-8.
  

2.3 Uchaguzi wa Jogoo Bora wa Mbegu

 

Jogoo wa mbegu anatakiwa awe na sifa zifuatazo:-

 
  • Achaguliwe kutoka kwenye koo zenye sifa ya kutaga mayai
  • mengi,
  •  Mrefu, umbo kubwa, miguu imara na yenye nguvu,
  •  Awe machachari, ushawishi kwa mitetea na ari ya kupanda
  • Uwezo wa kupanda akiwa na umri wa miezi 7-10.
 

3.0 Mayai kwa Ajili ya Kutotoa Vifaranga

 

3.1 Uchaguzi wa Mayai

 

Mayai kwa ajili ya kutotoa vifaranga yawe na sifa zifuatazo:-

 

• Yaliyorutubishwa na jogoo,

 

• Yasiwe na nyufa,

 

• Yasiwe na maganda tepetepe,

 

• Yasiwe na kiini kilichovunjika,

 

• Yawe na ukubwa wa wastani; na

 

• Yasiwe yamekaa zaidi ya wiki 2 baada ya kutagwa.

  

3.2 Utunzaji wa Mayai

 

Mayai ya kienyeji kwa ajili ya kutotoa vifaranga yatunzwe kwa  kusimamishwa wima sehemu iliyochongoka ikiwa imeangalia chini kwa siku

 

3 za mwanzo na kisha yageuzwe ili sehemu iliyobutu iangalie chini. Mayai

 

yahifadhiwe kwenye sehemu iliyo na ubaridi kidogo na giza.

   

4. Utunzaji wa Kuku kwa Makundi

 

1. Utunzaji wa Vifaranga

 

Malezi bora ya vifaranga ni muhimu katika ufugaji wa kuku kwa sababu vifaranga hawana uwezo wa kustahimili mazingira wakiwa wenyewe mara

 

wanapoanguliwa.Ukosefu wa malezi bora husababisha vifaranga kuwa dhaifu,kufa kwa wingi na hivyo kupunguza idadi ya kuku wa baadaye. Malezi ya vifaranga yanaweza kufanyika kwa kutumia kuku walezi au kutumia vifaa maalum.

  
  • Kulea Vifaranga kwa Kutumia Kuku Mlezi
 

Vifaranga wanaweza kulelewa na mama yao au kuku mlezi. Endapo kuku

 

wengi wametotoa vifaranga kwa wakati mmoja, achaguliwe kuku mlezi aliye na uwezo wa kulea vifaranga wengi kati ya waliototoa aendelee kulea

 

na wengine waliototoa waachwe huru ili warudi kwenye mzunguko wa kutaga. Kuku mmoja anaweza kulea vifaranga 20 hadi 25. Mfugaji wa kuku,pamoja na kanuni nyingine, anapaswa kuzingatia yafuatayo:-

 
  • Kuku anayelea vifaranga atengewe chumba maalumu, apewe maji ya
  • kutosha na chakula chenye virutubisho muhimu,
  • Vifaranga wasiachiwe kutoka nje hadi watakapofika umri wa wiki 6,
  • Vifaranga watengwe na mama/mlezi baada ya wiki 4 kuruhusu mama
  • aendelee na mzunguko wa kutaga;na
  • Katika maeneo yenye hali ya hewa ya ubaridi vifaranga
  • wacheleweshwe kutenganishwa na mama/mlezi hadi wiki ya 6 au mpaka waonekane wameota manyoya ya kutosha
  • Kulea Vifaranga kwa Kutumia Bruda
 

Bruda ni chombo/sehemu iliyoandaliwa mahusus kwa ajili ya kuwapatia joto vifaranga badala ya mama/mlezi. Mfugaji anaweza kulea vifaranga wengi kwa kutumia bruda ambayo ni mduara unaweza kutengenezwa kwa

 

kutumia mbao, karatasi ngumu au kwa kuziba pembe za chumba.Aidha, njia hii hupunguza vifo vya vifaranga vinavyosababishwa na ndege au wanyama hatari,huruhusu kuku kutaga mapema zaidi na kuwa na mizunguko mingi ya utagaji (kwa kuku wanaoatamia). Vilevile, hurahisisha

 

udhibiti wa magonjwa.

  

Mfugaji anapaswa kufuata taratibu zifuatazo katika kulea vifaranga kwa

 

kutumia bruda:-

 
  • Kuweka vifaa vya kuongeza joto kwa mfano taa ya umeme, chemli au   jiko la mkaa. Zingatia kiwango cha joto kinachohitajika katika bruda.
 

Wiki ya kwanza ni 35oc, wiki ya pili ni 33oc, wiki ya tatu ni 31oc na

 

wiki ya nne ni 29oc,

  
  • Kuchunguza mtawanyiko wa vifaranga ndani ya bruda ili kutathimini hali ya joto.Wakijikusanya kwenye chanzo cha joto, inaashiria kuwa baridi imezidi hivyo joto liongezwe. Wakiwa mbali na chanzo cha joto maana yake joto limezidi hivyo joto lipunguzwe,
  • Bruda iwe na sakafu yenye malalo yatokanayo na maranda ya mbao au pumba za mpunga. Malalo yabadilishwe endapo yataonekana yameloana,
  • Bruda iwekwe vifaa vya maji na chakula. Maji na chakula kiwekwe kabla ya kuweka vifaranga,
  • Vifaa vya joto viwekwe ndani ya bruda masaa 6 kabla ya kuingiza vifaranga,
  • Vifaranga walishwe chakula cha kuanzia gramu 12-15 kwa kipindi cha wiki ya 2. Katika wiki ya 3 wapewe gramu 21-35 kwa kifaranga na chakula hicho kiwepo muda wote,
  • Vifaranga wapatiwe vitamin, madini na dawa za kinga (antibiotics); na
  • Vifaranga wapatiwe chanjo kulingana na maelekezo ya mtaalamu wa mifugo.Chanjo dhidi ya magonjwa muhimu kwa mfano,Marek’s (mara anapototolewa), Mdondo (siku ya 3-4 na kurudiwa baada ya siku ya 21 na kila baada ya miezi 3) na Gumboro (siku ya 7na kurudia tena siku ya 21).Wapatiwa dawa ya minyoo (wiki ya 8) na coccidiosis(wiki ya 3-4). Siku ya 45 wapewe chanjo ya ndui ya kuku.
  

2. Kutunza Kuku Wanaokua (Wiki 8-18)

 

Utunzaji wa kundi hili unategemea mfumo unaotumika. Kuku Wanaofugwa Katika Mfumo Huria Kuku wanaofugwa katika mfumo huu wapatiwe matunzo bora yakiwemo yafuatayo;

  

Wapewe chakula cha ziada asubuhi kabla ya kutoka na wanaporudi kwenye banda. Chakula hicho kinaweza kugawanywa mara ya 2 kwa siku,

 
  • Wapatiwe maji safi na ya kutosha wakati wote
  • Wapatiwe chanjo na dawa kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo. Wiki ya kumi warudie chanjo ya mdondo, wiki ya 12 kuhara (fowl cholera), wiki ya 14 ndui ya kuku,
  

Kuku Wanaofugwa Katika Mfumo Shadidi

 
  • Majogoo watenganishwe na mitetea katika wiki 7 hadi 10 ili kuzuia uzaliano usio na mpangilio,
  • Wapewe chakula cha kukuzia kuanzia wiki ya 8-15 gramu 55- 60 na kuanzia wiki ya 16 gramu 65-80 kwa wanaofugwa mfumo huria na gram 120-125 kwa kuku kwa siku kwa wanaofugwa mfumo wa shadidi,
  • Kuku wa nyama wapatiwe chakula cha kuku wa nyama muda wote,
  • Wapatiwe maji safi ya kunywa kwa muda wote kwenye vyombo safi,
  • Kuku wachunguzwe dalili zozote za ugonjwa ili waweze kupata tiba sahihi kutoka kwa mtalaamu wa mifugo,
  • Kuku wa wiki 9-20 wanahitaji nafasi ya mita za mraba 0.15 kwa kuku na wiki 21 au zaidi mita za mraba 0.2 kwa kuku,
  • Kuwe na vyombo maalum vya kutosha kwa ajili ya chakula na maji,
  • Wafanyiwe usafi wa banda mara kwa mara ili kuzuia magonjwa yanayotokana na uchafu.
  • Wakatwe midomo ili kuzuia kudonoana.
 

3. Kuku Wanaotaga

 

Mahitaji ya kuku wanaotaga ni tofauti na makundi mengine

 

Mambo ya kuzingatia kwa kuku wanaotaga ni pamoja na:-

 
  • Banda liwe na viota vya kutagia mayai (kiota 1 kwa kuku 3-5).Viota viwekwe bandani mara kuku watakapofikisha umri wa wiki 18 ili waanze kuzoea kuvitumia,
  • Wapatiwe chakula na maji safi wakati wote kwa kutumia vyombo maalum ambavyo ni visafi,
  • Kuku wasiotaga waondolewe kwenye kundi.Kuku hao huonekana wasafi na sehemu ya kutolea yai huwa ndogo na kavu,upanga wake kichwa (comb) huwa mdogo na mwekundu,
  • Wapatiwe dawa ya minyoo kila baada ya miezi 3,
  • Wawekewe fito au ubao mwembamba kama sehemu ya kupumzikia na mazoezi ili kuzuia kudonoana,
  • Mayai yakusanywe mara 4 au zaidi kwa siku ili yasidonolewe na kuku,
  • Kuwe na malalo makavu na yabadilishwe mara yanapochafuka,
  • Vyombo vifanyiwe usafi kila ili kuzuia magonjwa; na
  • Watundikiwe majani mabichi aina ya mchicha,papai, alfaafa,majani jamii ya mikunde ili kuboresha lishe.
  

5.0 Udhibiti na Tiba Dhidi ya Magonjwa ya Kuku

 

Kuku wanaopata lishe bora, kutunzwa vizuri na kupatiwa chanjo dhidi ya magonjwa yanayotokea mara kwa mara huwa na afya nzuri. Ni bora kuzuia magonjwa kuliko kutibu ili kupunguza vifo na gharama. Iwapo ugonjwa utatokea kuku wagonjwa watenganishwe na kuku wasio wagonjwa na wapatiwe tiba. Kanuni muhimu za kufuata ili kuzuia magonjwa ni:-

 
  • Banda liwe safi muda wote,
  • Kabla ya kuweka kuku, banda linyunyuziwe dawa ya kuua wadau wa magonjwa mbalimbali,
  • Kuku wakaguliwe kila siku ili kubaini wagonjwa au wenye matatizo, kuwatenga na kutoa taarifa kwa mtaalam wa mifugo,
  • Kuku wapatiwe chanjo dhidi ya magonjwa mbalimbali,
  • Watu wasiohusika wasiingie eneo la kufugia kuku bila utaratibu,
  • Ndege na wanyama wengine wasifike eneo la kufugia kuku,
  • Banda la kufugia kuku litenganishwe na mabanda ya mifugo mingine,
  • Lango la kuingia katika banda la kuku liwekewe dawa ya kukanyaga kwa wanaoingia ndani ili kuzuia kuingiza vimelea vya wadudu wa magonjwa;na
  • Vifaa vya chakula na maji viwe safi wakati wote.
   

Dalili za Kuku Mgonjwa

 

Dalili za ujumla zinazoonekana kwa kuku mgonjwa ni kama zifuatazo:-

 
  • Kuzubaa,
  • Kupoteza hamu ya kula,
  • Kujitenga na wenzake katika kundi; na
  • Kupunguza au kusimama kutaga.
 

NB: Mfugaji anapoona mojawapo ya dalili hizo atoe taarifa kwa mtaalum wa mifugo.

  

6.0 Utunzaji wa Kumbukumbu

 

Utunzaji wa kumbukumbu ni muhimu sana katika ufugaji wa kuku na ndege wengine wafugwao ili kusaidia mfugaji kujua maendeleo ya ufugaji wake. Utaratibu wa kuweka kumbukumbu mara tukio linapotokea ni lazima ili kuepuka kusahau.Mfugaji ahakikishe anaweka kumbukumbu ambazo ni sahihi na zinazoeleweka.

  

Aina za Kumbukumbu

 

Kumbukumbu zinazopaswa kuwekwa ni pamoja na:-

 
  • Aina na idadi ya kuku waliopo kwenye kila kundi (mfano vifaranga,wanaokua,wanaotaga,majogoo),
  • Uzalishaji wa mayai kwa kundi la kuku waliopo,
  • Utotoaji wa vifaranga,
  • Kinga na matibabu,
  • Mapato na matumizi,
  • Utagaji wa kila kuku na utunzaji (kwa kuku wa asili); na
  • Kumbukumbu za vifo.
  

7.0 Chakula na uchanganyaji wake

 

Chakula ndicho huchangia sana katika gharama za uzalishaji kwa zaidi ya asilimia 60. Na gharama ya chakula huongezeka kila mwaka kuliko hata gharama za mayai au kuku wenyewe. Mfugaji anaweza kununua chakula kilichochanganywa au kuchanganya mwenyewe. Ila anapaswa kuzingatia virutubisho na viini lishe vilivyopo katika chakula hicho pia kuzingatia mahitaji ya kuku wake.

  

Virutubisho vinavyotakiwa ni vingi lakini vimegawanywa katika makundi sita ya vyakula ambavyo ni; protin, wanga, mafuta, madini,vitamini na maji.

  

Protini inahitajika kujenga mwili wa kuku. Ni muhimu kwa ukuaji wa kuku, uzalishaji wa mayai na kuimarisha afya. Wanga na mafuta vinahitajika ili kuupa mwili nguvu na joto na kuwezesha mwili kufanya kazi zake ipasavyo. Vitamini vinahitajika ili kumwezesha mwili wa kuku kufanya kazi zake vizuri. Madini yanahitajika ili kuimarisha mifupa na uzalishaji.

 

 

 

Kwa msaada wa ushauri wa ufugaji wa kuku, Wasiliana na wataalam wa mifugo walio karibu nawe

 


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA MASASI DC 2025 January 14, 2025
  • MGAWANYO WA MAENEO YA UTAWALA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA TAREHE 27 NOVEMBA, 2024 MASASI DC September 18, 2024
  • MAENEO YA UTAWALA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI September 18, 2024
  • FURSA YA MIKOPO INAYOTOLEWA NA MFUKO WA MIKOPO KUTOKA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI November 12, 2021
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • WATENDAJI WA SERIKALI TEKELEZENI WAJIBU WENU WA KIKAZI,MSIJIHUSISHE NA MAMBO YA SIASA: BARAZA LA MADIWANI

    May 15, 2025
  • WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI NA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO ILI KUFANIKISHA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA AWAMU YA PILI.

    May 15, 2025
  • WATAALAMU MASASI DC WAPATIWA MAFUNZO YA MATUMIZI YA MFUMO WA UJIBUJI HOJA ZA CAG.

    May 11, 2025
  • KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO YATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO ROBO YA III (JAN -MACHI 2025) INAYOTEKELEZWA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI.

    May 06, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

KAIMU MKURUGENZI MASUMBUKO MTESIGWA AKABIZI OFISI KWA MKURUGENZI MPYA
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • RASIMU YA MPANGO WA BAJETI KWA MWAKA WA FWDHA 2021/2022 MASASI DC
  • Mpango Mkakati wa halmashauri ya wilaya ya masasi 2016/2017-2020/2021
  • Taarifa ya Hesabu ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2015/16
  • Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 Masasi DC
  • Uchunguzi wa Madai ya Korosho kwa Misimu ya 2016/17 NA 2017/18 Wilaya ya Masasi
  • Mpango Kzazi wa Manunuzi kwa mwaka wa Fedha 2017-2018 Masasi DC
  • Mwongozo wa Malalamiko
  • Sheria

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Mtwara Region
  • Hati ya Malipo (Salary Slip)
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya Ajira
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Masasi - Bomani

    Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi

    Simu ya mezani: 023-2510031

    Simu ya kiganjani: 023-2510031

    Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa