Bi Changwa Mohamed Mkwazu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Masasi kuanzia tarehe 12/07/2016
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Masasi alizaliwa tarehe 27.03.1967 wilayani Kwimba ambayo hivi sasa ipo wilaya ya Misungwi Mwanza. Bi. Changwa Mohamed Mkwazu ameolewa na anao watoto wawili.
Kazi:
Mwaka 1990 hadi 1996 alikuwa mwalimu katika Shule ya Sekondari ya Ufundi Tanga (Tanga Technical Secondary School) akifundisha masomo ya Hisabati na Fizikia. Mnamo mwaka 1996 – 2003 alifundisha Shule ya Sekondari Kambangwa D’Salaam. Na kuanzia mwaka 2003 hadi 2016 alifundisha Shule ya Sekondari Mtakuja Beach iliyopo D’Salaam akiwa pia Makamu Mkuu wa Shule kuanzia mwaka 2006 hadi 2016. Pia alikuwa mwalimu wa Taaluma kuanzia mwaka 2000 hadi 2003.
Elimu:
Bi. Changwa Mohamed Mkwazu alipata Elimu ya Msingi katika Shule ya Msingi Kilimo – Ukinguni (Mwanza) kuanzia mwaka 1975 hadi 1977 baadae alihamishiwa Shule ya Msingi Kimange (Mkoa wa Pwani) kuanzia mwaka 1977 hadi 1982 alijiunga na Shule ya Sekondari Highlands iliyopo Mkoa wa Iringa na baadae kidato cha tano na sita katika Chuo cha Elimu Mkwawa ambapo alipata pia stashahada ya ualimu mnamo mwaka 1990.
Bi. Changwa Mohamed Mkwazu alijiunga na Jeshi la kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria Mgambo – Tanga kuanzia Julai 1990 hadi July 1991. Kati ya mwaka 2003 hadi 2006 alijiunga na masomo ya stashahada (Advance Diploma) ya Menejimenti ya Rasilimali watu katika Chuo cha Ustawi wa Jamii Dar es Salaam, na baadae mwaka 2007 – 2009 alijiunga na Chuo Kikuu Mzumbe kambi ya Dar es Salaam kwa masomo ya shahada ya uzamili ya usimamizi wa masuala ya biashara na mashirika ya umma na kwa mwaka huo huo alifanya shahada ya uzamili ya sayansi ya Maendeleo ya Jamii Kiuchumi katika Chuo Kikuu cha The Southern New Hampshire cha Marekani ikishirikiana na Chuo Kikuu Huria cha Dar es Salaam.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa